Israel yaizuia boti ya wanaharakati kufika Ukanda wa Gaza

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imesema katika ujumbe wa mitandao ya kijamii kuwa boti hiyo inaelekea kwenye fukwe za Israel na abiria wake wako salama na wanatarajiwa kurejea katika nchi zao. Ilisema msaada wa kibinadamu uliobebwa kwenye boti hiyo utapelekwa Gaza kupitia njia zilizowekwa.

Muungano wa Freedom Flotilla, ambao ulikuwa umeandaa safari ya kupeleka misaada ya kibinadamu huko Gaza na kupinga hatua ya Israel ya kuuzingira Ukanda huo wa Wapalestina, ulisema wanaharakati hao “walitekwa nyara na wanajeshi wa Israel”. Mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg ni miongoni mwa wanaharakati 12 waliokuwemo kwenye boti hiyo kwa jina Madleen, ambayo ilifunga safari kutoka kisiwa cha Sicily nchini Italia wiki moja iliyopita. Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz aliliamuru jeshi siku ya Jumapili kuizuia boti hiyo ya Madleen kufika Gaza, akiutaja ujumbe huo wa kibinaadamu kuwa ni juhudi za propaganda za kuunga mkono Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *