Israel yaendelea kumwaga damu za Wapalestina Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina wengine wawili katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu, wakati wakiendelea na kampeni ya kijeshi ambayo imeifanya kambi ya wakimbizi ya Jenin “kutoweza kukalika”.