
Rais wa Israeli siku ya Jumanne, Machi 25, amesema “kushtushwa” kuona kwamba suala la mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza halikuwa tena miongoni mwa vipaumbele vya nchi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Nimeshtushwa sana kuona jinsi ghafla suala la mateka haliko tena kwenye orodha ya kipaumbele au habari,” Isaac Herzog amesema katika video iliyotolewa na ofisi yake. Amesisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi za “kuwarudisha mateka nyumbani, hadi mwisho.”
Jeshi la Israel latoa amri mpya kwa wakazi kuondoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel siku ya Jumanne limewaamuru wakaazi wa miji yote ya mpakani ya kaskazini kuhama, likisema maroketi ya Wapalestina yamerushwa ndani ya Israeli kutoka eneo hilo.
“Kwa usalama wenu, lazima muondoke na muelekee kusini mara moja kwenye maeneo salama yanayojulikana,” jeshi limewaamuru wakaazi wa Jabalia, kambi kubwa zaidi ya wakimbizi ya kihistoria ya Gaza.
Mashambulizi ya Israeli yawauwa watu 23 huko Gaza
Mashambulizi ya Israeli yamewauwa Wapalestina 23 katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumanne, kulingana na maafisa wa afya wa eneo hilo, huku jeshi la Israeli likitoa maagizo mapya ya kuhama kwa makumi ya maelfu ya wakaazi wa eneo hilo.