
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu, Machi 24, amemshutumu mkuu wa Shin Bet, ambaye kutimuliwa kwake Ijumaa kulizuiwa na Mahakama ya Juu, kwa kumchunguza Waziri wa Usalama wa taifa kutoka mrengo mkali wa kulia Itamar Ben Gvir bila ridhaa yake.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Madai kwamba Waziri Mkuu aliidhinisha mkuu wa Shin Bet Ronen Bar kukusanya ushahidi dhidi ya Waziri Ben Gvir ni uwongo mwingine ambao umefichuliwa,” imesema taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu katika kujibu kuchapishwa kwa ripoti ya Channel 12, ambayo imesema idara ya usalama wa ndani (Shin Bet) ilikuwa ikifanya “uchunguzi wa siri” kwa miezi kadhaa kuhusu kuingizwa kwa siri katika polisi kwa watu kutoka mrengo wa kulia na kwenye wizara ya Usalama wa Taifa.
Uamuzi ambao ulichochea hasira za upinzani
Katika tangazo lake wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Israeli alizungumza juu ya “kupoteza kwa uaminifu wa kitaaluma na kibinafsi.” Waziri Mkuu kupoteza imani kwa mkuu wa idara ya usalama wa ndani […] iliimarishwa wakati wa vita, mbali na kushindwa kufanya kazi Oktoba 7, na hasa katika miezi ya hivi karibuni,” alisema katika barua. Uamuzi huu uliamsha hasira za upinzani na kusababisha maandamano ya kulaani “tishio kwa demokrasia” na kumshutumu Waziri Mkuu kwa “kujilimbikizia” mamlaka.
Siku ya Alhamisi jioni, maelfu kadhaa ya watu walisimama kwenye mvua na upepo kuandamana nje ya makazi ya kibinafsi ya Benjamin Netanyahu huko Jerusalem, na kisha nje ya Knesset, bunge la Israeli, ambapo mawaziri walikuwa wakikutana.