
Israel imesema itaruhusu kuingizwa kwa misaada ya chakula muhimu kwenye ukanda wa Gaza, hatua inayomaliza miezi kadhaa ya zuio ambalo limewaweka raia wa Kipalestina kwenye hali mbaya ya njaa, wakati huu pia ikiendelea kupokea shinikizo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, hatua hiyo imechukuliwa baada ya tathmini ya wanajeshi wake ambao wameanzisha tena oparesheni kwenye ukanda wa Gaza.
Israel imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kuondoa zuio la misaada kuingia Gaza ambapo chakula, mafuta wala dawa havikuruhusiwa kuingia kwenye eneo hilo.
Mashirika ya misaada yameonya kuwa raia zaidi ya Milioni mbili kwenye Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na tishio la baa la njaa kutokana na hatua ya Israel.
Naye Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Noel Barrot ameitaka Israel kuhakiksha mashirika ya misaada yanaruhusiwa kuingia Gaza bila vizuizi.