Israel inasema itaendelea na mapigano hadi Hamas iwaachie mateka wote

Israel imeapa kuendelea na mapigano katika Ukanda wa Gaza hadi pale ambapo mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas wataachia huru.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la Israel limekuja wakati huu ikitekeleza mojawapo ya mashambulio mazito zaidi katika Ukanda wa Gaza tangu kaunza kwa kipindi cha usitishaji wa mapigano.

Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza imesema zaidi ya watu 330 wameuawa katika shambulio hilo la Israel.

Hamas imemtuhumu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuamua kurejelea mapigano baada ya kipindi cha usitishaji wa vita kupata muafaka wa kumaliza mzozo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. © BASHAR TALEB / AFP

Hamas imeonya kwamba kurejelewa kwa mapigano kutapelekea kuuawa kwa mateka wa Israeli ambao bado wako hai na wanazuiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Hili ndilo shambulio kubwa na baya zaidi tangu kuafikiwa kwa makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano tarehe 19 ya mwezi Januari.

Netanyahu aliwaonya wapiganaji wa Hamas mwezi huu kwamba watawajibishwa iwapo hawatowaachia huru mateka ambao wangali wanazuiliwa Gaza.

Misiri imelaani mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Misiri imelaani mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza. © Amir Cohen / Reuters

Ikulu ya Marekani imesema Israel ilipata ushauri kutoka kwa utawala wa rais wa Marekani Donald Trump kabla ya kutekeleza mashambulio hayo ambayo wizara ya afya ya katika ukanda wa Gaza inasema wengi waliouawa ni wanawake na watoto.

Ofisi ya Netanyahu imesema oparesheni hiyo iliagizwa baada ya Hamas mara kwa mara kuendelea kukataa kuwaachia mateka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *