Israel imewauwa shahidi Wapalestina zaidi ya 100 huko Gaza licha ya tangazo la usitishaji vita

Idara ya Ulinzi wa Raia ya Gaza imetangaza leo Ijumaa kuwa Wapalestina wasiopungua 101, wakiwemo watoto 27 na wanawake 31, wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel tangu kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano juzi Jumatano.