Israel imeshaua Wapalestina 40 Ghaza tangu baada ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha vita

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeendeleza mashambulio katika Ukanda wa Ghaza licha ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya utawala huo ghasibu na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS. Hadi wakati huu, Wapalestina wasiopungua 40 wameshauliwa shahidi na jeshi hilo.