Israel haitaondoa askari wake kusini mwa Lebanon kama ilivyoafikiwa, Marekani yaiunga mkono

Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halitaondoka kusini mwa Lebanon utakapomalizika muhula uliowekwa wa siku 60 kesho Jumapili kulingana na makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa kati ya Israel na harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah.