IRGC yazindua kituo kipya cha chini ya ardhi cha makombora ya kruzi ya kuteketeza manowari za mashambulizi

Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua kituo kipya cha chini ya ardhi katika maeneo ya mwambao wa kusini mwa Iran, kinachohifadhi makombora yaliyo tayari kuteketeza manowari za mashambulizi za adui katika eneo la kimkakati la majini.