IRGC yapokea manowari ya kisasa iliyoundwa na wataalamu wa Iran (ASUBUHI)

Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimepokea zana na vifaa mbalimbali vya kijeshi vilivyoundwa na kutengenezwa hapa nchini Iran, ikiwemo meli ya kivita ya Shahidi Rais Ali Delvari na makumi ya meli za mashambulizi ya haraka zenye mifumo ya kurusha makombora.