IRGC: Hatua yoyote ya Israel dhidi ya Iran itakabaliwa na majibu makubwa zaidi

Kamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba iwapo Wazayuni watachukua “hatua kubwa” dhidi ya Iran, bila shaka watakabiliwa na jibu kubwa “mara kadhaa zaidi”.

“Jibu la Iran litategemea ukubwa wa mashambulizi ya adui. Iwapo hatua muhimu itachukuliwa, jibu litakuwa kubwa mara kadhaa,” amesema Meja Jenerali Mohammad Ali Ja’fari, akizungumza kando ya hafla ya kumbukumbu ya mshauri wa kijeshi wa Iran nchini Lebanon, shahidi Meja Jenerali Abbas Nilforoushan.

Israel ilimuua shahidi Nilforoushan na kiongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, kusini mwa Beirut tarehe 27 Septemba.

“Ninawahakikishia watu wa Iran kwa yakini kwamba, Wazayuni hawatachukua hatua yoyote muhimu au kubwa; chochote watakachofanya kitakuwa jaribio la kukata tamaa.”

“Utawala wa Kizayuni unaweza kufanya shambulio la kukata tamaa, dhaifu, na dogo,” Ja’fari amesema, akisisitiza kwamba “lakini kwa hakika hauwezi” kutekeleza operesheni inayolingana na Operesheni Ahadi ya Kweli II ya Iran.

Mnamo Oktoba 1, IRGC ilirusha mamia ya makombora ya balestiki ya dhidi ya kambi za jeshi, vituo vya ujasusi na taasisi za kiintelijensia za utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu na kusababisha uharibifu mkubwa.

Operesheni hiyo ilitekkelezwa kulipiza kisasi mauaji ya Israel dhidi ya Nilforoushan pamoja na viongozi wa Hamas na Hizbullah.