Iran yatishia kushambulia kambi za Marekani

Nasirzadeh amesema taifa lake litakuwa tayari kushambulia kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika kanda ya Mashariki ya Kati iwapo mgogoro utatokea baada ya kushindwa kufikia mkataba wa nyklia na Marekani.

Ameyasema hayo kuelekea duru ya sita ya mazungumzo hayo ya nyuklia kati ya mahasimu hao wa muda mrefu. Marekani imesema mazungumzo hayo yatafanyika siku ya Alhamisi wiki hii huku Iran ikisema mazungumzo yatafanyika siku ya Jumapili nchini Oman.

Iran yaituhumu Marekani kuhujumu mazungumzo ya Nyuklia

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa vitisho mara kadhaa kwa Iran kuwa ataishambulia kwa mabomu iwapo hawatafikia mkataba huo wa nyuklia. 

Hata hivyo Aziz Nasirzadeh amesema hivi karibuni Iran ilifanya jaribio la makombora yake na haitakubali kamwe kudhibitiwa. Kiongozi Mkuu wa taifa hilo  Ayatollah Ali Khamenei alisema mwezi Februari kwamba Jamhuri hiyo inapaswa kuendelea kuimarisha jeshi lake ikiwa ni pamoja na makombora yake. 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *