
Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia baadhi ya matukio ya sayansi na teknolojia nchini Iran na maeneo mengine duniani. Ni matumaini yangu kuwa utaweza kunufaika.
Hossein Mozdarani, mshiriki wa kitivo cha idara ya sayansi ya matibabu katika Chuo Kikuu cha Tarbiat Modarres cha Tehran, Iran ameshinda ‘Tuzo la Mafanikio ya Maisha’ kutoka Shirikisho la Asia-Oceania la Mashirika ya Fizikia ya Matibabu (AFOMP).
Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya AFOMP hutunukiwa kila mwaka katika Mkutano wa Asia-Oceania wa Fizikia ya Matibabu (AOCMP) kwa mwanafizikia wa matibabu aliyechaguliwa na Kamati ya Tuzo na Heshima ya AFOMP (AHC). Anayepata tuzo hii huwa ameonyesha mchango mkubwa kwa fizikia ya matibabu na jamii katika eneo la Shirikisho la Asia-Oceania la Mashirika ya Fizikia ya Matibabu (AFOMP).
Mozdarani amechaguliwa kutoka kwa zaidi ya wateule 40 kwa kutambua utafiti wake wa miaka 30 na maendeleo ya biolojia ya redio nchini Iran na nchi nyingine za eneo la Asia Oceania, shirika la habari la Mehr liliripoti.
Zawadi hiyo ilitolewa kwake katika hafla ya kufunga AOCMP ya 24 na Congress ya 22 ya Asia ya Kusini-Mashariki ya Fizikia ya Tiba (SEACOMP) iliyofanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 13 huko Penang, Malaysia.
Mkutano wa Asia-Oceania wa Fizikia ya Matibabu na ule wa eneo la Asia ya Kusini-Mashariki ya Fizikia ya Tiba ni matukio muhimu ya kila mwaka katika fizikia ya matibabu barani Asia. Madhumuni ni kukusanya fizikia ya matibabu na wataalamu wa afya washirika katika eneo ili kubadilishana maarifa, utaalamu, mijadala ya kisayansi, kubadilishana utamaduni na masasisho ya teknolojia ya matibabu.
Mwaka huu, mkutano ulifanyika chini ya kaulimbiu ya ‘Kubadilisha Huduma ya Wagonjwa kupitia Fizikia ya Tiba’.
Zaidi ya washiriki 500 kutoka taaluma ya fizikia ya matibabu, uhandisi wa matibabu, radiolojia, radiotherapy, dawa ya nyuklia, ulinzi wa mionzi, biofizikia, radiobiolojia, na nyanja zinazohusiana walihudhuria hafla hiyo.
Kampuni zinazotegemea maarifa au Knowledge based nchini Iran
Idadi ya kampuni zinazotegemea maarifa au Knowledge based nchini Iran ambazo zinafanya kazi katika sekta ya afya zimekaribia kuongezeka mara mbili kutoka 762 katika mwaka wa kalenda 2021-2022 hadi 1,501 katika mwaka wa sasa wa Irani ulioanza Machi 20.
Kampuni zinazotegemea maarifa zinafanya kazi kwa kujumuisha sayansi na utajiri, kukuza uchumi unaotegemea maarifa, kufikia malengo ya kisayansi na kiuchumi, na vile vile kufanya utafiti na maendeleo ya kibiashara katika nyanja ya afya.
Yunes Panahi, naibu waziri wa afya Iran amesema hivi sasa, kampuni zinazotegemea maarifa katika sekta ya afya zinafanya kazi katika nyanja mbalimbali zikiwemo kilimo, teknolojia ya kibayoteknolojia, na tasnia ya chakula, dawa, na zana za matibabu na utafiti wa hali ya juu, pamoja na vifaa vya matibabu.
Ukuaji mkubwa na wa haraka wa idadi ya kampuni zinazotegemea maarifa na ongezeko la zaidi ya asilimia 200 katika idadi yao katika mwaka uliopita unaonyesha msingi thabiti na ukuaji wa nchi katika uvumbuzi, teknolojia na mazingira ya uzalishaji ambayo yamepatikana kwa kuzingatia lengo la kukuza uzalishaji wa ndani kwa ushirikishwaji wa umma.
Mnamo Januari 13, mkuu wa Muungano wa Watengenezaji na Wasafirishaji wa Vifaa vya Tiba nchini Iran alisema kuwa vifaa vya matibabu vyenye thamani ya karibu dola milioni 20 vinasafirishwa kwa zaidi ya nchi 60 kila mwaka.
Olympiad ya Kimataifa katika Akili Mnemba
Ali Sharifi-Zarchi, profesa wa akili mnemba au artificial intelligence na bioinformatiki katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif cha Iran, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kisayansi ya Olympiad ya Kimataifa katika Akili Mnemba (IOAI).
Olympiad ya Kimataifa katika Akili Mnemba ndilo shindano la kila mwaka la kifahari zaidi katika uga wa Akili Mnemba kwa wanafunzi wa shule za upili. Dhamira yake ni kuhamasisha na kutoa changamoto vijana kuchunguza matumizi yasiyo na kikomo ya Akili Mnemba na kuangazia mustakabali wa sekta hiyo.
Olympiad ya Kimataifa katika Aki Mnemba ni shindano linalolenga Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati kwa kifupi STEM ili kuhamasisha, kuendeleza, na kukuza wanafunzi bora katika Akili Mnemba duniani kote.
Kama Olympiad ya Akili Mnemba, Olympiad ya Kimataifa katika Aki Mnemba itashiriki kikamilifu katika majadiliano na umma kwa ujumla kuhusu vipengele vya maadili na mustakabali wa Akili Mnemba.
Waanzilishi pia wanalenga kuhusisha mtu mashuhuri kila mwaka ili kukuza ya Olympiad ya Kimataifa katika Akili Mnemba , na pamoja na wanafunzi kuhamasisha mazungumzo mapana ya jamii kuhusu Akili Mnemba.
Toleo la 1 la ya Olympiad ya Kimataifa katika Aki Mnemba lilifanyika Burgas, Bulgaria mnamo Agosti 2024.
Jumla ya timu 41 kutoka nchi 30 zilishiriki katika raundi 2 za shindano hilio.
Timu ya taifa ya Iran ilipata mafanikio ya ajabu katika Mashindano ya kwanza ya Olympiad ya Kimataifa katika Akili Mnemba, na kupata medali ya timu ya shaba na kupata daraja la 18 katika tukio hilo lililofanyika nchini Bulgaria.
Timu hiyo, iliyojumuisha wanafunzi Mohammad Sadra Kouhestani, Amir Hossein Zarei, Parsa Sadeghi, na Alireza Rahimi Yazdi, walionyesha ujuzi wao katika mazingira yenye ushindani mkubwa.
Katika mojawapo ya changamoto tatu za kisayansi, timu ya Iran ilitoa suluhu bora zaidi kati ya timu 41 zilizoshiriki kutoka nchi 33, na kuonyesha usahihi ambao uliwazidi washindani wao tu bali pia suluhu lililotolewa na mbuni wa tatizo hilo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Iran.
Olympiad ya Pili ua Kimataifa katika Akili Mnemba ya 2025 itafanyika Beijing, Uchina, katika msimu wa joto.