Iran yaonya: Shambulio dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia litasababisha ‘vita vitakavyoenea katika eneo’

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ametoa onyo kali kuhusu matokeo mabaya ya kitendo cha uchokozi kinachoweza kufanywa, ambacho kinaweza kuuhusisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.