Iran yaonya baada ya Israel kutishia kushambulia ndege yake ya abiria

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei ameukosoa vikali utawala wa Kizayuni Israel kwa kutishia kushambulia ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa imebeba raia wa Lebanon.