Iran yamweleza Guterres: UN ichukue msimamo thabiti kuhusu njama ya Trump dhidi ya Palestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi amesema Umoja wa Mataifa, hasa Baraza lake la Usalama, lazima uchukue msimamo “imara na wa wazi” dhidi ya mpango wa Marekani na Israel unaolenga kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza.