Iran yalipiza kisasi dhidi ya Israeli kwa kurusha makumi ya makombora ya balistiki

Saa 24 baada ya Israeli kufanya mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya miundombinu ya kijeshi na nyuklia ya Iran na jibu la Iran kwa kurusha makombora ya balistiki dhidi ya taifa la Kiyahudi, mvutano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kushika kasi. Usiku wa Ijumaa, Juni 13, kuamkia Jumamosi, Juni 14, mlipuko ulisikika katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Mehrabad wa Tehran, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran imefanya mashambulizi mapya dhidi ya Israeli mapema Jumamosi asubuhi, baada ya jeshi la Israeli kuripoti kutambua kurusha makombora kutoka ardhi ya Iran. “Msururu mpya wa mashambulizi kama sehemu ya Operesheni Honest Promise 3” ulizinduliwa, televisheni ya serikali imeripoti.

Wakati Waziri Mkuu wa Israeli akizindua kampeni isiyo na kifani ya mashambulizi dhidi ya Iran usiku wa Alhamisi, Juni 12 kuamkia Ijumaa, Juni 13, Waisraeli wanauchukuliaje mpango huu? Je, wanamuunga mkono Benjamin Netanyahu, ambaye anadai anataka kuizuia Tehran kupata silaha za nyuklia na kuwa tishio kwa taifa la Kiyahudi? Alice Moreno, mmoja wa waandishi wa RFI mjini Jerusalem, alikwenda kuwauliza wakaazi wa mji huo mtakatifu. Wengi hawakuchukulia sahihi mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran.

“Inatosha, ni wakati wa kusitisha uhasama,” anashutumusema mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa Iran na Israeli kukomesha mashambulizi na kusitisha uhasama kufuatia mabadilishano kadhaa ya mashambulizi ya mabomu  yanayofanywa na nchi moja dhidi ya nyingine. 

“Mashambulio ya Israeli katika maeneo ya nyuklia ya Iran” 

Iran yafanya mashambulizi ya mabomu katika mji wa Tel Aviv. Inatosha kwa mashambulizi haya, ni wakati wa kukomesha uhasama.” “Amani na diplomasia lazima viwepo,” anasema Antonio Guterres kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *