
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani vikali shambulio la kigaidi kwenye makao makuu ya Shirika la Anga la Uturuki (TOSASH) mjini Ankara.
Jana Jumatano, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki ilitangaza shambulio la kigaidi dhidi ya kampuni ya anga ya nchi hiyo mjini Ankara. Katika shambulio hilo, watu watatu waliuawa na watu 14 walijeruhiwa. Washambuliaji wote wawili waliuawa baada ya makabiliano na vikosi vya usalama vya Uturuki.
Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya Sahab, ikimukuu shirika la habari la Mehr, Ismail Beqaei, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali shambulio la kigaidi kwenye makao makuu ya Shirika la Anga la Uturuki (Tosash) mjini Ankara.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga, wananchi na serikali rafiki na jirani ya Uturuki kufuatia tukio hilo la kigaidi, na kulaani vikali ugaidi wa kila namna.
Msemaji huyo wa chombo cha diplomasia cha Iran amesisitiza pia utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kushirikiana na nchi nyingine hususan nchi jirani katika kupambana na ugaidi.