Iran yakanusha kuwasaidia Wahouthi baada ya shambulio kwenye uwanja wa ndege wa Israeli

Iran siku ya Jumatatu, Mei 5, imekanusha kutoa msaada kwa waasi wa Houthi wa Yemen, ambao wamedai kuhusika na shambulio la kombora kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv, uwanja mkuu wa kimataifa wa Israeli, kwa jina la kutetea Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Hatua ya Yemen ya kuunga mkono watu wa Palestina ni uamuzi huru uliofanywa kwa mshikamano” na Wapalestina, Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa.

Iran inawaunga mkono Wahouthi, ambao wamedhibiti maeneo makubwa ya Yemen iliyokumbwa na vita tangu mwaka 2014.

Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya waasi wa Houthi na Iran kwa kile alichosema kuwa wanaunga mkono waasi.

“Israeli itajibu shambulio (hili) la Houthi (…) NA kwa wakati ufaao na mahali tulipochagua, kwa wakuu wao wa magaidi wa Iran,” meandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Ikijibu vitisho hivi, Iran imehakikisha Jumatatu kwamba italipiza kisasi dhidi ya shambulio lolote dhidi ya ardhi yake.

“Iran inasisitiza azimio lake thabiti (…) la kujilinda,” taarifa ya kidiplomasia ya Iran imesema, ikionya Israeli na Marekani kuhusu “matokeo” ya mashambulizi yanayoweza kutokea.

Rais wa Marekani Donald Trump na utawala wake wameongeza vitisho vyao dhidi ya Iran katika miezi ya hivi karibuni kwa kuwaunga mkono Wahouthi.

Shambulio hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv siku ya Jumapili lilisababisha kusitishwa kwa muda kwa safari za ndege na kusababisha watu sita kujeruhiwa kidogo, kulingana na mamlaka ya Israeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *