Iran yaionya Israel kutokariri mauaji ya kimbari ya Gaza katika Ukingo wa Magharibi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameitolea wito jamii ya kimataifa kuishurutisha Israel isikariri jinai yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kama ilivyofanya katika Ukanda wa Gaza.