Iran yaiambia EU: Kwanza jifunzeni maana ya ’tishio’ na ‘amani’ ndipo muwatuhumu wengine

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeushauri Umoja wa Ulaya kwenda kujifunza kwanza maana ya “tishio” , “amani” na “usalama wa kimataifa” kabla ya kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu kwa madai chapwa ya kutishia usalama wa kimataifa.