Iran: Uingereza inaendeleza siasa za kindumilakuwili kuhusu ugaidi

Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London umeilaumu Uingereza kwa siasa zake za nyuso mbili kuhusu ugaidi na kusema kuwa, wakati wananchi wa Iran wanapouawa kigaidi, kwa mujibu wa serikali ya London, ugaidi huo unavumilika, na hauwezi kuchukuliwa msimamo kama wa ugaidi unaofanyika maeneo mengine.