Iran: Ni muhimu kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kuwahami wanawake na watoto wa Gaza na Lebanon

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya wanawake na familia amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kuwahami na kuwasaidia wanawake na watoto wa Gaza na Lebanon.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza haya katika Mkutano wa Kamisheni ya Kiuchumi na Kijamii wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Asia ya Kusini na Oceania huko Thailand (ESCAP). 

Bi Zahra Behrouz Azar amekosoa upuuzaji na kimya cha jamii ya kimataifa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika Ukanda wa Gaza na Lebanon.  

Bi Azar ameashiria umuhimu wa maadhimisho ya mwaka wa 30 tangu kupasishwa Hati ya Beijing na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikichukua hatua za kuboresha hadhi ya wanawake kwa kuzingatia misingi ya Katiba na mafundisho ya Kiislamu.

Mkutano wa ESCAP nchini Thailand 

Mkutano wa ESCAP ulianza Jumanne Novemba 19 katika Kituo cha Mikutano cha Umoja wa Mataifa mjini Bangkok, Thailand na utaendelea hadi siku ya Alhamisi.