Iran: Mustakbali bora wa Ulimwengu wa Kiislamu ndiyo sababu ya kuimarishwa uhusiano wetu na Saudia

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Riyadh amesema kwa mnasaba wa kutimia mwaka mmoja tangu nchi mbili za Iran na Saudia zirejeshe uhusiano wao wa kidiplomasia kwamba, lengo la Tehran katika kuimarisha uhusiano wake na Saudi Arabia ni kuyaletea manufaa mataifa haya mawili ya Kiislamu na kuuandalia umma wa Kiislamu mustakbali bora.