Iran: Miezi 15 ya jinai za wavamizi huko Ghaza isingewezekana bila ya msaada wa Marekani na Magharibi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa, sambamba na kusitishwa mauaji ya kimbari huko Ghaza, jumuiya ya kimataifa inapaswa kukabiliana kwa umakini na ipasavyo uasi wa utawala wa Kizayuni katika eneo lote la Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Inabidi kuandaliwe pia uwanja wa kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kuadhibiwa viongozi magaidi wa utawala katili wa Israel kwa jinai za kivita.