
Kutokana na vikwazo vikali vya Marekani na Ulaya, Iran imeamua kununua dhahabu kwa wingi, ambayo ni kimbilio salama.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi
Mkuu wa Benki Kuu amesema hadi wezi Oktoba mwaka uliyopita, Iran ilikuwa imebadilisha 20% ya akiba yake ya fedha za kigeni kwa dhahabu, iliyonunuliwa kwenye masoko ya kimataifa. “Sisi ni miongoni mwa wanunuzi watano wakubwa wa dhahabu duniani,” ameongeza.
Sababu ni rahisi. Iran ndiyo nchi duniani yenye vikwazo vingi zaidi vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.
Rais wa Marekani Donald Trump amezidi kuimarisha vikwazo hivi kwa kutoa agizo la kiutendaji linalolenga kutekeleza sera ya shinikizo la juu, haswa kuzuia mauzo yote ya mafuta kutoka Iran na kuilazimisha Tehran kuweka kikomo mpango wake wa nyuklia.
Washington imemuongeza hivi punde Waziri wa Mafuta Mohsen Paknejad kwenye orodha yake ya vikwazo. Lakini pia makampuni 18 na meli 13 au meli za mafuta. Sera hiyo inalenga kukata baadhi ya ufadhili wa utawala wa “kukomesha tishio la nyuklia linaloletwa na Iran, kuzuia mpango wake wa makombora ya balestiki, na kuizuia kuunga mkono au kuanzisha tena makundi ya kigaidi yanyofanya kazi kwa maslahi yake,” utawala wa Trump unadai.
Benki za Iran hazina uhusiano na benki za kigeni na hazina ufikiaji wa mtandao wa Swift, mfumo wa ujumbe wa kubadilishana baina ya benki.
Kutokana na vikwazo vya Marekani, fedha nyingi za Iran zimezuiwa nje ya nchi, zikiwemo dola bilioni sita nchini Qatar na dola bilioni kadhaa nchini Iraq na China. Hii inaeleza kwa nini Iran imeamua kugeukia dhahabu, ambayo ni kimbilio salama na ambayo thamani yake inaendelea kuongezeka duniani kote.