Iran: Kuruka ndege za Israel jijini Beirut wakati wa mazishi ya Shahidi Nasrallah ni “kitendo cha ugaidi”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amelaani hatua ya ndege za kivita za utawala haramu wa Israel kuruka juu ya uwanja wa michezo nchini Lebanon, ambako shughuli za mazishi ya viongozi wa Hizbullah waliouawa shahdii zilikuwa zinafanyika, akitaja tukio hilo kama “kitendo cha ugaidi” kilicholenga kuwatisha waombolezaji.