
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, sababu kuu ya kiburi na ufidhuli wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani.
Ismail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari hapa mjini Tehran na kubainisha kuwa, viongozi wa Marekani wanapaswa kusimamisha uungaji mmokono na misaada yao ya kisilaha, kijasusi na kisiasa kwa utawala huo ghasibu.
Akiashiria hatua ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushambulia Iran siku ya Jumamosi, Ismail Baqaei ameeleza kuwa, nukta muhimu katika shambuulio la Jumamosi la Israel ni kudhihirika bayana uwezo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Aidha amesema kuhusiana na jinai za Israel kwamba: Mashauriano yote yaliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika wiki za hivi karibuni yalilenga kusitishwa mara moja jinai za Israel dhidi ya Gaza na Lebanon, uhamasishaji wa jamii ya kimataifa kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi na kujaribu kuuwajibisha utawala wa Kizayuni kwa sababu tunaamini kwamba, kutochuukuua kwetu hatua za kisheria dhidi ya Israel ndiko kulikoutia kiburi na kuupa kichwa utawala huo ghhasibu.