
Mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameishtumu Marekani kwa kuhusika katika mashambulizi ya Israeli dhidi ya nchi yake siku ya Ijumaa, madai ambayo Washington imekanusha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akishutumu taifa la Kiyahudi kwa kutaka “kuua diplomasia, kuhujumu mazungumzo, na kuliingiza eneo hilo kwenye mgogoro mpana,” Amir Saeed Iravani pia amesema kwamba ushirikiano wa Washington ulikuwa “hauna shaka.” “Wale wanaounga mkono utawala huu [utawala wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu], unaoongozwa na Marekani, lazima waelewe kwamba wao ni washiriki,” amesema na kuongeza: “Kwa kusaidia na kuunga mkono uhalifu huu, wanashiriki wajibu kamili kwa matokeo yao.”
Moshi mnene na miali ya moto kwenye Uwanja wa Ndege wa Mehrabad wa Tehran
Moto mkubwa ulizuka katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Mehrabad mjini Tehran, ambapo moshi mkubwa umefuka, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP katika mji mkuu wa Iran. Eneo hilo pia zinahifadhiwa ndege za kivita za Iran, anaripoti mwandishi wa RFI Siavosh Ghazi, ambaye anaongeza kuwa maeneo mengine ya jiji pia yamelengwa, pamoja na miji ya Karaj na Isfahan.
Nchini Syria, Washia wagawanyika kati ya mshikamano na Iran na hofu ya vita vipya
Mshirika wa zamani wa Tehran, Syria pia inapakana na Israeli, ambayo inakalia Milima ya Golan kusini magharibi mwake. Nchini humo, jumuiya ya Kishia inafuatilia kukithiri kwa uhasama kati yya dola ya Kiyahudi na Jamhuri ya Kiislamu na hivyo kusababisha wasiwasi fulani, kama inavyoonyeshwa na ripoti hii kutoka Damascus na Mohamed Errami, mwandishi wa RFI, ambaye pia alikusanya ushuhuda wa simu kutoka kwa baadhi ya wakazi wa Daraa.
Wakati huo huo mamlaka ya Israeli imepunguza kiwango cha tahadhari nchini kote usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, na kuruhusu raia kuwa wanaweza kuondoka kwenye makazi yao mradi wangebaki “karibu”. Maagizo hayo mapya yametolewa takriban dakika ishirini baada ya kutangazwa kwa makombora mapya ya Iran katika taifa la Kiyahudi.