
Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh anasema hujuma ya hivi majuzi wa utawala wa Israel dhidi ya vituo kadhaa vya kijeshi vya Iran ulisababisha uharibifu “mdogo” ambao ulirekebishwa mara moja.
Nasirzadeh aliyasema hayo katika hotuba kwa wanafunzi wasio Wairani wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Ulinzi cha Juu na wambata wa kijeshi wa kigeni wanaoishi Tehran siku ya Jumatatu.
Amesema ukarabati huo ulitekelezwa kwa kutumia ujuzi na uwezo wetu wa kisayansi wa wataalamu Waraini.
Amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel umekiuka kanuni zote za kimataifa ambazo zinalenga kutetea haki za binadamu na uadilifu.
Utawala wa Israel ulishambulia vituo kadhaa vya kijeshi vya Iran mapema Jumamosi, na kuua wanajeshi wanne wa Jeshi na raia mmoja.
Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Iran kimetangaza kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini sababu iliyopelekea adui kutekeleza uharibifu huo mdogo
Kwingineko katika maelezo yake, Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema uwepo wa Marekani katika maeneo yote ya dunia, ikiwemo Bahari ya Kusini ya China na uchochezi wake kuhusu Taiwan, njia za kimataifa kama vile Mlango-Bahari wa Bab el-Mandab na kuchochea vita kati ya Russia na Ukraine, ni mambo ambayo yanalenga ubabe wa Marekani.
Mkuu huyo wa ulinzi wa Iran amezitaka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu zinazotafuta haki kutumia nguvu na umakini wao wa kisayansi kujiimarisha.