Iran: Hatutaki vita, lakini tutajihami kwa nguvu zote

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa: Hatufurahishwi na vita na machafuko na wala hatupendi, lakini iwapo adui ataanzisha vita dhidi yetu basi bila ya shaka tutailinda Iran kwa nguvu zetu zote na kutoa jibu kali kwa maadui.