Iran: Fedheha ya Zelensky nchini Marekani, kengele ya hatari ya kurejea ubabe wa karne ya 19

Iran imesema mwenendo wa kudhalilisha wa Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, katika Ikulu ya White House unapaswa kuwa “kengele ya hatari” ya kurejea kwenye zama za karne ya 19 za uonevu na utumiaji mabavu katika uhusiano wa kimataifa.