Iran: Baraza la Qur’ani la Ulimwengu wa Kiisilamu litasahilisha uhusiano na ushirikiano baina ya Waislamu

Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran amesema: “kuundwa Baraza la Qur’ani la Ulimwengu wa Kiislamu kunaweza kusahilisha ujengaji wa uhusiano na kubadilishana tajiriba kwa ajili ya ushirikiano kati ya Waislamu.”