IOM: Vita vya Sudan vimeongeza idadi ya wakimbizi wa ndani Pembe ya Afrika

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema idadi ya wakimbizi wa ndani (IDP) katika Pembe ya Afrika iliongezeka hadi milioni 20.75 kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2024.