
“Sudan Kusini iko katika ukingo wa vita vipya vikubwa,” linaonya Shirika la Kimataifa linalotatua migogoro International Crisis Group (ICG), ambalo lina wasiwasi kuhusu kuzuka kwa ghasia mpya nchini humo. Mnamo Machi 4, 2025, wanamgambo wa Nuer wanaohusishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar, waliteka kambi ya kijeshi huko Nasir, mji ulio kwenye mpaka na Ethiopia.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hali hiyo ya hatari inatishia, kwa mujibu wa ripoti hiyo, “serikali dhaifu ya umoja iliunda chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2018 ambao ulimaliza miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.” ICG inasema matukio haya yatakuwa madhara ya moja kwa moja ya mzozo katika nchi jirani ya Sudani.
Kulingana na ripoti ya ICG, “mvutano uko katika kilele chake katika mji mkuu, Juba.” Kwa wiki kadhaa, Sudani Kusini imekuwa uwanja wa mabadiliko ya kisiasa ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo inatishia kusambaratisha makubaliano ya amani ya mwaka 2018.
“Mapato ya mafuta yameporomoka”
Lawama zinatokana na vita nchini Sudani na hasa kukatwa kwa bomba linalotumika kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini kwenda Bandari ya Sudan, kulingana na Daniel Akech, mchambuzi katika ICG. “Hali imebadilika hivi karibuni kwa sababu, katika mwaka uliopita, mapato ya mafuta yameporomoka kutokana na vita nchini Sudani. Hii imefanya iwe vigumu kwa serikali kulipa mishahara yake. Hapa ndipo tatizo linapoanzia. “
Akiwa ametengwa na chanzo chake kikuu cha fedha ambacho kilikuwa kinahudumia mtandao wake wa wateja, na kwa hivyo utulivu wa serikali yake, Salva Kiir hivi karibuni alisogea karibu na Jenerali Hemidti, mkuu wa RSF, na hivyo kujiweka mbali na Jenerali al-Burhan, mkuu wa jeshi la Sudani. Wanamgambo hao wanasemekana kuamsha uhusiano wa zamani na wanamgambo wa Nuer wanaoshirikiana na Riek Machar huko Upper Nile.
Kukamatwa kwa kambi ya jeshi
Hali ambayo ilisababisha, Machi 4, kutekwa kwa kambi ya kijeshi katika mji wa Nasir na kundi la wanamgambo wa White Army, linaloshirikiana na Riek Machar, ambao wengi wa wafuasi wake walikamatwa baadaye. Wakati makamu wa rais amekaa kimya kwa sasa, Daniel Akech anaonya kuwa wanamgambo wanaomtii hawako mbali na mji mkuu wa Sudan Kusini.