Inonga aleta kizaazaa Yanga, mabosi wagawanyika

DILI la beki wa kati wa zamani wa Simba anayekipiga FAR Rabat ya Morocco, Henock Inonga kutua Yanga limeibua mvutano mkali baada ya kutokea mgawanyiko kwa mabosi wa klabu hiyo, huku baadhi wakitaka asisajiliwe.

Katika hoja mbili zinazovutana juu ya dili hilo, wanaosema asisajiliwe wanasisitiza kwa sasa hawataki kuona wanamsajili mchezaji ambaye amepita Simba, huku wale waliopendekeza asajiliwe wanasimamia kwenye msimamo wao kwamba ni mchezaji mzuri atawasaidia.

Hivi karibuni, Mwanaspoti lilikujuza kwamba Yanga iko mbioni kufanya makubaliano na Mkongomani huyo aliyewahi kuitumikia Simba kabla ya kutimkia FAR Rabat ya Morocco aliko sasa.

Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, ishu mpya ni kwamba mabosi wa klabu hiyo wamegawanyika, huku wengine wakitaka usajili huo ufanyik

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *