
India imefanya mashambulizi katika mikoa mitatu ya Pakistani usiku wa Jumanne, Mei 6, kuamkia Jumatano, Mei 7, jeshi la Pakistani limetangaza, likitaja miji miwili ya Kashmir ya Pakistani na wa tatu huko Punjab kati ya miji iliyolengwa.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
New Delhi, kwa upande wake, inadai kushambulia “miundombinu ya kigaidi” na imeyaita mashambulizi yake “Operation Sindoor”. Pakistani imejibu kwa kufyatua mizinga katika eneo la India.
Milipuko imesikika katika maeneo kadhaa ya Pakistani, shule za Punjab zimefungwa
Mashambulizi ya India, ambayo New Delhi inayaita Operation Sindoor, yamelenga maeneo kadhaa ya Pakistani. Jeshi la Pakistani awali lilitaja maeneo matatu yaliyolengwa. Kulingana na ripoti kutokamaeneo ya mapigano, milipuko ilitokea katika angalau maeneo matano ya Pakistani, huko Kashmir na Punjab. Mojawapo ya maeneo yaliyolengwa mara moja na jeshi la India ni Msikiti wa Subhan huko Bahawalpur, katika Punjab ya Pakistani, ambayo kulingana na ujasusi wa India unahusishwa na makundi yaliyo karibu na LeT, haswa Jaish-e-Mohammed (JeM). Mara moja, serikali ya jimbo hili, ambapo karibu nusu ya watu milioni 240 wa Pakistani wanaishi, imetangaza kufungwa kwa shule zote Jumatano.
India imearifu Marekani baada ya mashambulio yake nchini Pakistani
Ubalozi wa India huko Washington umesema Mshauri wa Usalama wa taifa wa India Ajit Doval amemweleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio baada ya mashambulizi ya jeshi la India nchini Pakistani. “Hatua za India zimelengwa kw sahihi,” ubalozi umesema.
“Dunia haiwezi kuvumilia makabiliano ya kijeshi” kati ya India na Pakistan, Umoja wa Mataifa unabainisha
“Ulimwengu hauwezi kuvumilia makabiliano ya kijeshi” kati ya India na Pakistani, amesema msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), muda mfupi baada ya mashambulizi ya kijeshi kati ya New Delhi na Islamabad. Katibu Mkuu Antonio Guterres “anatoa wito kwa nchi zote mbili kujizuia kijeshi,” msemaji wake, Stéphane Dujarric ameongeza katika taarifa.
Pakistani yakutana na Kamati yake ya Usalama wa taifa
Pakistani itaitisha Kamati yake ya Usalama wa taifa siku ya Jumatano saa 11:00 alfajiri, Waziri wa Habari Ataullah Tarar ametangaza. Baraza hili, linaloundwa na maafisa wakuu wa kiraia na kijeshi, hukutana tu katika hali mbaya zaidi, katikati ya kuongezeka mgogoro wa kijeshi na India. Mnamo Aprili 24, kamati ilitangaza msururu wa vikwazo vya kidiplomasia dhidi ya India kulipiza kisasi kwa hatua kama hizo zilizochukuliwa na New Delhi muda mfupi baada ya shambulio baya huko Kashmir ambalo India inailaumu Pakistani.
Raia watatu waliouawa na mashambulizi ya India, atangaza Waziri wa Ulinzi wa Pakistani
Raia watatu, akiwemo mtoto, wameuawa katika mashambulizi ya India ya “kuwalenga raia,” Waziri wa Ulinzi wa Pakistani Khawaja Asif ameliambia shirika la habari la AFP. “Tumethibitisha ripoti za raia watatu waliouawa, akiwemo mtoto,” amesema, akiongeza kwamba India “imelenga maeneo mengi, yote ya raia.”
Donald Trump anatumai kwamba mapigano kati ya India na Pakistani “yatasitishwa haraka sana”
Rais wa Marekani ndiye kiongozi wa kwanza mwenye hadhi ya juu kujibu uhasama kati ya India na Pakistani. Kutoka Washington, Donald Trumpme: “Ni aibu. Unajua, wamekuwa wakipigana kwa miongo na karne nyingi, kwa kweli, ikiwa unafikiria juu yake. Natumai mapigano haya yatasitishwa hivi karibuni.