India: Watu sita wauawa baada ya mapigano Kashmir

Maafisa wanne wa polisi na watu wawili wanaoshukiwa kuwa waasi wameuawa katika eneo la India la Kashmir, ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa serikali ya kitaifa ya Narendra Modi tangu mwaka 2019 na limekuwa likikumbwa na uasi wa kujitenga kwa miongo kadhaa, shirika la habari la AFP linaripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika chapisho la mtandao wa kijamii Jumamosi, Machi 29, Jeshi la India la Rising Star Corps limesema “operesheni kali” imesababisha “kuangamizwa kwa magaidi wawili,” neno linalotumiwa sana na India kurejelea waasi wanaopinga udhibiti wa New Delhi wa Kashmir.

Mapigano hayo yalianza Alhamisi katika eneo lenye misitu la Kathua kusini mwa Kashmir wakati askari wa doria walipovamiwa walipokuwa wakitafuta waasi, na kuua polisi wanne, mkuu wa polisi Nalin Prabhat amewaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa jioni.

Baadaye Nalin Prabhat amedai kuwa wanamgambo waliouawa walitoka Pakistan, bila kutoa maelezo zaidi juu ya utambulisho wao.

Kashmir yenye Waislamu wengi inadaiwa kwa ujumla wake na India na Pakistan, nchi mbili zenye nguvu za nyuklia ambazo kila moja inadhibiti sehemu ya eneo hilo.

“Hatutapumzika hadi tukomeshe shughuli za jirani yetu,” mkuu wa polisi wa India amesema.

India mara kwa mara inashutumu Pakistani kwa kutuma waasi kuvuka mpaka usio rasmi na wenye silaha kali ili kuanzisha mashambulizi dhidi ya majeshi ya India.

Islamabad inakanusha shutuma hizo, ikisema inaunga mkono tu mapambano ya Kashmir ya kujitawala.

India inadumisha takriban wanajeshi nusu milioni waliowekwa kwa muda wa kudumu katika eneo ambalo makundi yenye silaha yamepigania kwa miongo kadhaa kwa ajili ya uhuru wa Kashmir au unyakuzi wake na Pakistani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *