India: BRICS haina msimamo wa pamoja kuhusu suala la kuachana na sarafu ya dola ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar amesema, dhana ya kwamba kundi la mataifa ya BRICS linafanya juu chini kukabiliana na sarafu ya dola ya Marekani “haijathibitishwa na ukweli” na akaongeza kuwa, India hasa kwa upande wake “haina nia hata kidogo ya kuidhoofisha sarafu hiyo.