Imeelezwa kuwa tatizo sugu la foleni katika barabara za jiji la Dar es Salaam linaweza kuongeza msongo wa mawazo kwa watumiaji w…

Imeelezwa kuwa tatizo sugu la foleni katika barabara za jiji la Dar es Salaam linaweza kuongeza msongo wa mawazo kwa watumiaji w…

Imeelezwa kuwa tatizo sugu la foleni katika barabara za jiji la Dar es Salaam linaweza kuongeza msongo wa mawazo kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri, kuchochea uchovu kwa madereva na abiria na hatimaye kuongeza uwezekano wa ajali na vifo barabarani.

Hayo yamebainika katika wiki ambayo jiji hilo limekumbwa na misongamano mikubwa kwenye barabara kuu mbalimbali, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi.

Mwandishi wetu Joseph Mpangala amezungumza na wananchi katika maeneo tofauti ya jiji hilo, akishuhudia namna foleni hizi zinavyoathiri maisha na shughuli za kila siku za wakazi wa Dar es Salaam.

#azamnewsupdates
✍@joempangala
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *