Ikulu ya White House inajaribu kutuliza mzozo baada ya kutolewa kwa taarifa za kijeshi

Utawala wa rais Donald Trump umeendesha mashambulizi siku ya Jumanne, Machi 25, huku kesi ya mwandishi wa habari wa Jarida la Atlantic ambaye alipokea taarifa za siri kuhusu operesheni za kijeshi ikiendelea kushika kasi. Maafisa wa usalama wa kitaifa wamehojiwa katika Bunge la Congress bila kufanikiwa kuwashawishi, pia kuwatia wasiwasi maafisa waliochaguliwa kutoka chama cha Republican.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Wakati Ikulu ya White House inajaribu kupuuzi suala hilo la uvujaji wa taarifa za jeshi, wabunge kutoka chama cha Democratic wanaomba waliohusika katika kashfa hiyo wajiuzulu.

Wabunge wa chama cha Democratic wanaahidi kutokata tamaa. Katika barua kwa Donald Trump, kiongozi wa wachache wa Baraza la Wawakilishi, kama wenzake wengi, ametoa wito wa kujiuzulu kwa mkuu wa Pentagon kufuatia kufichuliwa kwa jambo hilo, anaripoti mwandishi wetu huko New York, Loubna Anaki. “Pete Hegseth ndiye Waziri wa Ulinzi asiye na uwezo zaidi katika historia ya Marekani,” Hakeem Jeffries almeandika katika barua yake kwa rais. Anamshutumu Waziri wa Ulinzi kwa “kufanya kazi kwa upole na uzembe kwa kushiriki mipango ya kina ya vita kwenye kikundi cha mazungumzo kisicho salama.”

Wabunge wa chama cha Democratic pia wanataka kujiuzulu kwa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Mike Waltz, ambaye aliunda kikundi cha mazungumzo kwenye programu ya Signal. Wabunge wachache wa chama cha Republican wamejiunga na wakosoaji wakitaka uchunguzi wa ndani ufanyike, ili “kuzuia kashfa kama hiyo isirudi tena kutokea.”

Sio wazi kuwa suala hilo linaishia hapo, kwani mwandishi wa habari wa Jarida la The Atlantiki amedokeza kuwa ana habari zaidi ya kufichua.

Kwa upande wake, Ikulu ya Marekani inajaribu kupuuzia suala hilo. Kwenye kituo cha habari cha Fox News, Mike Waltz alisemame jukumu kamili, akikubali kwamba aliunda kikundi cha mazungumzo lakini akisisitiza kuwa hajui jinsi mwandishi wa habari wa jarida la The Atlantiki alipatikana katika kikundi hiki. “Sasa inabidi tuendelee na masuala mengine,”me.

Trump anaongelea hitilafu isiyo na uzito wowote

Rais wa Marekani, ambaye aliingia madarakani mwezi Januari, amesema katika simu na NBC kwamba “ilikuwa hitilafu pekee ndani ya miezi miwili, na hatimaye sio mbaya.”

Donald Trump kisha akamtangaza Jeffrey Goldberg, ambaye alifichua makosa hayo kuwa aliongezwa kimakosa kwenye kikundi cha mazungumzo cha maafisa wakuu wa Marekani, kuwa ni “tapeli.” Amesema kwamba “hakuna anayejali” kile Jarida la The Atlantic, ambayo Jeffrey Goldberg ni mhariri mkuu, linachapisha.

Kuhusiana na mshauri wake wa usalama wa taifa, Mike Waltz, rais amesema kuwa “anafanya kila awezalo” na “yeye ni mtu mzuri sana.” Donald Trump amesema wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Mike Waltz hakuwa na chochote cha kuomba msamaha.

“Ikiwa hapakuwa na taarifa za siri, kwa nini huwezi kushiriki mjadala?” “Hakukuwa na taarifa za siri zilizoshirikiwa,” amesema Mkurugenzi wa Ujasusi Tulsi Gabbard, ambaye alijkabiliwa na maswali mengi kutoka maseneta wa chama cha Democratic wakatika kikao cha Bunge la Seneti kilichopangwa kwa muda mrefu. “Ikiwa hapakuwa na taarifa za siri, kwa nini huwezi kushiriki mjadala mzima nasi? ” anauliza Seneta kutoka chama cha Democratic Mark Warner wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Tofauti na Tulsi Gabbard, mkuu wa CIA, John Ratcliffe alikiri kushiriki katika kitanzi hiki cha ujumbe. Alihojiwa wakati huo huo na Bi. Gabbard, lakini ametetea matumizi ya “kuidhinishwa na kisheria” ya maombi ya kubadilishana haya kati ya Makamu wa Rais J.D. Vance, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth na Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio miongoni mwa wengine.

Kesi hiyo inaonekana kuwa mkate uliojawa baraka kwa upinzani wa chama vha Democratic, ambao umetatizika hadi sasa kupata mwelekeo wa mashambulizi dhidi ya Donald Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *