IAEA: Tumekubaliana na Iran tuendeleze falsafa ya mapatano ya JCPOA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema katika mazungumzo na waandishi wa habari mjini Tokyo Japan kuwa: “Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwamba “falsafa ya JCPOA” ambayo msingi wake ni “kuchukua Iran hatua za hiari mkabala wa kupewa upendeleo na motisha,” inaweza kuendelea.