
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, amri ya kuhama ilioyotolewa na Israel katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza imefanywa kkwamadhumuni ya kuwatesa, kulazimishwa Wapalestina kuwa wakimbizi na kusambaa raia wa Palestina.
Human Rights Wacht imesema kuwa, hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni ni kielelezo cha wazi kabisa cha jinai dhidi ya binadamu.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema katika ripoti yake kwamba ushahidi unaonyesha uhalifu wa kivita wa kuwahamisha raia kwa nguvu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ukiukaji mkubwa wa Mikataba ya Geneva na uhalifu unaotokana na Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Roma. .
Human Rights Watch imetoa wito wa kuangaliwa upya sera ya kuwafanya Wapalestina kulazimika kuwa wakimbizi.
Shirika hilo la haki za binadamu limesema kuna haja ya kuwekwa vikwazo vyenye malengo dhidi ya Israel na sambamba na kutouziwa silaha utawala huo ambao umekuwa ukifanya mauaji kila uchao dhidi ya Wapalestina.
Hayo yanajiri katika hali ambayo wanajeshi wa Israel wameua shahidi zaidi ya raia 2,000 kaskazini mwa ukanda wa Gaza baada ya utawala huo ghasibu kuanzisha kampeni ya kuangamiza kabisa kila kitu cha eneo hilo tangu siku 38 zilizopita.