Marais wa DRC Felix Tshisekedi na wa Angola Joao Lorenco wamekutana jana mjini Luanda ambapo baada ya mkutano huo, serikali ya Luanda ilitangaza uwezekano wa kuanza kwa majadiliano ya moja kwa moja baina ya Kinshasa na waasi wa M23.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Ofisi ya rais wa Angola imesema hapo jana Jumanne kwamba itawasiliana na waasi wa M23 ili kuwezesha mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutafuta amani mashariki mwa DRC.
Tangazo hilo lilifuatia mkutano wa Luanda kati ya Rais wa Angola Joao Lourenco na Rais wa DRC Felix Tshisekedi. Hii ilikuwa ni ziara ya pili ya Tshisekedi nchini Angola kwa mazungumzo ya upatanishi wa amani ndani ya mwezi mmoja.

Serikali ya DRC imekuwa ikikataa katukatu haiwezi kuketi kwenye meza ya mazungumzo na waasi wa M23 na kuwatuhumu kuwa vibaraka wa Rwanda.
Tina Salama, msemaji wa rais wa DRC, alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba DRC inasubiri kutekelezwa kwa mpango wa upatanishi wa Angola.
Zaidi ya hayo, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ilitangaza kuwa itafanya mkutano wa kilele usio wa kawaida wa wakuu wa nchi na serikali siku ya Alhamisi kujadili hali ya usalama nchini DRC.
Mzozo unaoendelea kati ya waasi wa M23 na serikali ya DRC umesababisha idadi kubwa ya watu kuyahama makazi yao na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu. Mvutano bado uko juu licha ya juhudi za kidiplomasia na kijeshi kumaliza uhasama huo.

Jumatatu hii, Rais Lourenço pia alikutana na wawakilishi wa makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti huko Luanda.
Kwa upande wao, wanafanya mashauriano na wadau wote katika suala hili ili kukuza mazungumzo. Viongozi wa dini walisema wamepata uungwaji mkono wa rais wa Angola kwa mpango wao huo