Hofu yaibuliwa kuhusu vifo vya akina mama wajawazito

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hatua zilizopigwa katika kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua huenda zikatatizika kutokana na kupungua kwa ufadhili katika sekta ya afya duniani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua vilipungua kwa asilimia 40 katika kipindi cha mwaka wa 2000 hadi 2023.

Licha ya hatua zilizopigwa, wasiwasi umeibuliwa na wadau wa sekta ya afya kufuatia kupunguzwa kwa ufadhili wa shirika la afya duniani WHO lililokuwa linategemea pakubwa msaada toka kwa Marekani ambayo hivi karibuni imetangaza kusitisha misaada ya nje.

Mwaka 2023, karibia wanawake laki 2 na elfu 60 walifariki kutokana na changamoto za uzazi, kila baada ya dakika mbili.

Hivi karibuni, WHO ilionya kuwa kupunguzwa kwa ufadhili wa sekta ya afya duniani kutakuwa tishio katika vita dhidi ya maambukizo ya kifua kikuu na Ukimwi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *