
Wapiganaji wa harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon wameiangusha ndege ya kivita ya Israel isiyo na rubani ilipokuwa ikiruka angani juu ya wilaya ya Marjeyoun kusini mwa Lebanon karibu na mpaka na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu
Hizbullah imesema katika taarifa fupi kwamba, kitengo chake cha ulinzi wa anga kililenga ndege isiyo na rubani ya Hermes 450 kwa kombora la kutoka ardhini hadi angani siku ya Jumamosi.
Harakati hiyo ya muqawama pia lilivurumisha makombora tofauti katika mikusanyiko ya wanajeshi katili wa Israel katika eneo la kijeshi la al-Abad karibu na mpaka wa Lebanon, na pia katika makaazi haramu ya walowezi wa Kizayuni ya Manara.
Zaidi ya hayo, Hizbullah imetangaza kuhusika na shambulio la roketi dhidi ya makazi haramu ya walowezi wa Kizayuni ya Kiryat Shmona katika upande wa kaskazini wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Wapiganaji wa Hizbullah pia walishambulia ngome za walowezi wa Kizayuni za Baram na Maalot Tarshiha kwa makombora, na kusababisha uharibifu katika maeneo yaliyolengwa.
Pia siku ya Jumamosi, Hizbullah ililirusha roketi nyingi katika mji wa kaskazini unaokaliwa kwa mabavu wa Safed, na kulenga kambi ya viwanda vya kijeshi ya Zvulon kaskazini mwa Haifa kwa msururu wa maroketi.
Hizbullah imesema operesheni hizo zimefanywa kwa mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, kuunga mapambano yao shupavu dhidi ya utawala haramu wa Israel na pia kuilinda Lebanon.