Hizbullah ya Lebanon yafanya oparesheni 30 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imesema katika taarifa kwamba wanamapambano wake wamefanya oparesheni 30 tofauti siku ya Jumatatu dhidi ya utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Hizbullah imesema oparesheni za siku ya Jumatatu zililenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, ngome za jeshi, ndege, kambi na mikusanyiko ya wanajeshi kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel na kusini mwa Lebanon.

Oparesheni hizo zilitekelezwa kwa kutumia makombora, ndege zisizo na rubani, maroketi na mizinga na kulenga maeneo ya askari wa utawala wa Kizayuni katika mistari ya mawasiliano na karibu kabisa na ngome za adui Mzayuni.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa zaidi ya makombora 150 yalirushwa kutoka Lebanon siku ya Jumapili kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo pandikizi wa Israel.

Makombora hayo yalisababisha moto kuenea katika baadhi ya maeneo kikiwemo kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kiryat Shmona.

Silaha za wanamuqawama wa Hizbullah

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni, shambulio moja kubwa la kombora lilipiga Galilaya Magharibi.

Katika upande mwingine, kanali ya habari ya Al-Mayadeen iliripoti jana kuwa milipuko 40 ilisikika katika vitongoji tofauti vya walowezi wa Kizayuni na kambi za kijeshi.

Vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kuwa Hizbullah imelenga maeneo kadhaa ya Nahariyya na Magharibi mwa Galilaya kwa makombora zaidi ya 30 zenye uwezo mkubwa wa kutoa miripuko.

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa mashambulizi ya Hizbullah ya Lebanobn yamepelekea kutolewa amri ya kuwataka walowezi wa maeneo hayo wayahame makazi yao.

Hizbullah ya Lebanon haijakaa kimya mbele ya uvamizi na jinai za  kinyama zinazofanywa na utawala dhalimu wa  Israel. Harakati hiyo ya Muqawama imekuwa ikisisitiza katika taarifa yake mara kwa mara kuwa oparesheni zake zinatekelezwa kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kulinda mamlaka mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Lebanon.