Hivi ndivyo vituo vitatu vya anga za mbali vya Iran vilivyofelisha vikwazo vya Marekani

Licha ya kuweko vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, lakini vituo vitatu vya anga za mbali vya Iran vimeendelea kuzalisha teknolojia ya kisasa ya anga za juu. Kwa kutegemea ujuzi wa wananchi wake na uwezo wa wataalamu wa ndani ya Iran, vituo hivi vimefanikiwa kufelisha vikwazo na kupata maendeleo makubwa katika uwanja wa satelaiti na kurusha satelaiti kwenye anga za mbali.