Achana kabisa na pambano la Jumamosi ya Oktoba 19 mwaka huu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga. Achana matokeo ya kipigo cha bao 1-0 ilichopewa katia pambano hilo lililofanyika siku chache baada ya Mnyama kuwakera mashabiki kwa kiwango ilichokionyesha mbele ya Coastal Union.
Pambano hilo lilifanyika, huku mashabiki wa Mnyama wakijisahaulisha mapema zaidi kiwango cha timu yao dhidi ya Coastal Union waliofungana nao mabao 2-2, Wagosi wakichomoa baada ya kutanguliwa 2-0 kwa muda mrefu. Hii ilitokana na kulitazama Kundi A ililopangwa timu hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika ambayo michezo yake inaanza mwishoni mwa mwezi huu ya Novemba hadi Januari 19 mwakani.
Mnyama ana bahati mbaya. Ana mitihani mingi katika kundi hilo. Mtihani wa kwanza ni ukweli kwamba hivi karibuni mtani wa wa jadi, Yanga aliweka kipimo kizito kwake. Yanga na Simba si wanashindana kwa kila jambo? Ndio. Yanga alifika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika misimu miwili iliyopita.

Alicheza mechi mbili za fainali dhidi ya USMA Alger ya Algeria. Chochote ambacho kitatokea Mnyama asifike fainali za Shirikisho itaonekana amefeli vibaya. Hata akiishia nusu fainali itaonekana amefeli tu. Huu ni mlima mkubwa ambao Mnyama inabidi aupande. Tatizo mpira wenyewe haupo hivyo. Sio la
zima kila kitu kifanane au kila lengo lifanane.
Kitu kingine ni namna ambavyo watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wanavyoiangalia Simba. Ukimwambia shabiki wa Al Ahly kwamba Simba yupo katika kundi lenye timu za Bravos do Maquis ya Angola, CS Constantine ya Algeria na CS Sfaxien ya Tunisia atakwambia Simba ataongoza kundi. Huku ni kujichongea walikofanya ndani ya miaka mitano hii waliyotanua mbavu zao katika michuano ya CAF.
Na sasa ni zamu ya Simba kulipa haya madeni. Uzuri wa kwanza wa Simba katika hili ni kwamba wana-jua kuutumia uwanja wa nyumbani. Rafiki zetu kutoka Tripoli walithibitisha hilo wikiendi ile nyingine wakati walipochapwa mabao 3-1 pale Temeke, licha ya kucheza vyema katika pambano la kwanza nyumbani kwao. Kwa Mkapa hatoki mtu.

Mkononi kuna mechi tatu. Tuanze na hawa Waangola. Walicheza na Coastal Union hapo awali. Kwa macho yangu ni timu ya kawaida tu. Saizi ya Simba. Iwe Luanda au Temeke, Simba wanaweza kushinda mechi zao vizuri tu. Tatizo kubwa ni kwamba Simba bado wanajitafuta. Najisahau kuizungumzia Simba ninapoifikiria zaidi Simba ya Clatous Chama na Luis Miquissone. Najisahau.
Kwa Simba ile ningeweza kuweka shingo yangu na kisu kwamba Simba hakosi pointi nne au sita katika mechi mbili dhidi ya Bravos. Bahati mbaya Simba yangu hii haijanipa uhakika sana. Wachezaji wengi wapya, kocha mpya, tabia bado haijajengeka na kikosi hakijajengeka. Hata hivyo bado karata yangu ipo kwa Mnyama.
Tatizo kubwa la Mnyama lipo katika ukweli kwamba wamepewa watu wawili wa Afrika Kaskazini. Maji-rani Algeria na Tunisia. Twende pale Tunisia. Kuna Sfaxien. Moja kati ya timu kongwe katika soka la Af-rika, lakini imepotea katika miaka ya karibuni kiasi kwamba imewaruhusu kina Monastir kwenda mbele yao.
Sfaxien wapo katika hadhi sawa na kina Etoile Du Sahel na Esparance. Miongoni mwa timu ngumu ba-rani Afrika miaka hiyo. Hadhi sawa na kina Al Ahly, Waydad na Raja. Kabla ya kuibuka kwa hawa rafiki zetu Mamelodi ambao wamekuja kutokana na noti nzuri za Patrice Motsepe. Sfaxien wana mashabiki wa kutosha Tunisia.

Ardhi ya Afrika Kaskazini kupata pointi tatu kwa timu hizi kongwe ni kitu kigumu. Hata kwa timu za ka-waida ni kitu kigumu. Nakumbuka zamani kina Mohamed Mwameja waliwahi kushinda ugenini kule Afrika Kaskazini. Halafu Aziz Ki akawatungua Club Africain. Siyo kitu kinachojirudia mara nyingi.
Halafu kuna hawa CS Constantine. Hawa ni wababe wapya. Kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Algeria siyo jambo dogo. Ni moja kati ya ligi babe Afrika. Mnyama anapaswa kuwa makini na watu kama hawa. Sawa walianzishwa zamani, mwaka 1898 lakini hawajawahi kuwa tishio.
Mnyama ana mtihani mkubwa. Kinachonitia hofu ni namna ambavyo bado hawajajipata sana kama wa-tani zao. Hapa wana kazi mbili. Kuendelea kujipata huku wakilipa madeni ya watu. Yaani unaendelea kutafuta ‘chemistry’ nzuri katika timu huku unapata matokeo mazuri.
Kuna matokeo mazuri ya kuhakikisha Yanga hachukui ubingwa kwa mara ya nne mfululizo, huku pia ukijaribu kuhakikisha unatinga fainali za Shirikisho. Katika michuano hii ya Shirikisho, Simba kama walivyo watani wao Yanga wanahitaji kuhakikisha wana sare moja ugenini na kukusanya pointi tisa nyumbani.
Kama wakipata ushindi mmoja ugenini na pointi tisa nyumbani siyo mbaya. Hauwezi kufikisha pointi 10 au 12 katika kundi na usisonge mbele. Simba alishawahi kuongoza kundi la Al Ahly akiwa na pointi 15. Tatizo kuna wachezaji watatu tu wanaoweza kuanza katika timu ambayo ilifanya mambo yake.

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Shomari Kapombe na Mzamiru Yassin. Sahau kuhusu Aishi Manula. Kitu kingine ambacho ni silaha nzuri kwa Simba ni ukweli kwamba wanajitokeza uwanjani kwa wingi inapof-ika shughuli kama hii. Hawabaki nyumbani kama watani zao. Wamepitia kipindi kigumu hapa katikati lakini hawajawahi kuacha kuja uwanjani kumpa mpinzani wakati mgumu. Uwanja utakuwa wa moto kwa CS Constantine, Bravos na Sfaxien. Utakuwa wa moto kweli. Kinachotakiwa kwa sasa ni baadhi ya wachezaji kuendelea kusaka ufalme wao Simba.
Yusuf Kagoma fundi wa mpira. Abdulrazak Hamza, Leonel Ateba na Deborah Fernandes Mavambo wanaelekea kujivika ufalme katika nafasi nyingi amba-zo zipo wazo pale Simba. Awali kulikuwa na wachezaji wengi wa kawaida sana Simba ambao wame-furushwa. Na sasa kuna nafasi kubwa ya kujipatia ufalme mpya Msimbazi.
Tusubiri na kuona lakini bado nawapa nafasi Simba kupita kundi hili. Wana nafasi kubwa ya kuwathibit-ishia watu kwamba walitinga katika michuano hii kwa bahati mbaya tu. Hauwezi kutoka kuinyanyasa michuano ya Ligi ya Mabingwa halafu ukaangukia katika Shirikisho na kutolewa katika makundi.
Itashangaza. Kwa kipa, Moussa Camara nadhani anatakiwa kuwa makini zaidi. Fungate lake na masha-biki limefikia mwisho baada ya kufanya makosa mawili katika pambano dhidi ya Coastal Union ambayo yaliwarudisha Coastal Union uwanjani pale katika Uwanja wa KMC. Mpira wa Tanzania tunaufahamu wenyewe.